Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo Kampuni hiyo, Bw. Peter
Ngota akisisitiza umuhimu wa huduma mpya waandishi wa habari mfumo
mpya wa kibiashara na utendaji kwa ajili ya kuwapatia huduma bora wateja wake
kama njia ya kuchangia shughuli za maendeleo nchini kupitia huduma ya
mawasiliano ya simu jijini Dar es Salam jana. Kulia ni Meneja wa Kampuni
hiyo Dar es Salaam Kaskazini, Bwana Karim Bablia.
Meneja wa
Kampuni Kampuni ya Mawasiliano nchini (TTCL) Mkoa Dar es Salaam Kaskazini,
Bwana Karim Bablia akisisitiza umuhimu wa huduma mpya waandishi wa
habari mfumo mpya wa kibiashara na utendaji kwa ajili ya kuwapatia huduma bora
wateja wake kama njia ya kuchangia shughuli za maendeleo nchini kupitia huduma
ya mawasiliano ya simu jijini Dar es Salam jana.Kushoto Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo Kampuni
hiyo, Bw. Peter Ngota.
Na Mwandishi wetu,Dar es Salaam
Kampuni Kongwe ya Mawsiliano
Tanzania (TTCL) imeanzisha mfumo mpya wa kibiashara na utendaji kwa ajili ya
kuwapatia huduma bora wateja wake kama njia ya kuchangia shughuli za maendeleo
nchini kupitia huduma ya mawasiliano ya simu.
Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo Kampuni
hiyo, Bw. Peter Ngota aliwambia waandishi wa habari kuwa huduma hiyo itatoa
fursa kwa wateja wa kampuni hiyo ya serikali kupata huduma bora kupitia mfumo
huo.
“Mfumo huu ulianza kutumika Desemba Mosi
mwaka huu na ni muhimu katika kuwapatia wateja wetu huduma bora ambayo
inayokwenda na wakati,” aliongeza kusema Bw. Ngota.
Mfumo huu mpya wa wa kisasa wa mitandao ya
simu za mezani na mkononi ambapo sauti na data zinapatikana kupitia teknolojia
za CDM, GSM na LTE na kuongeza ubora wa huduma ya mawasiliano.
Alisema mfumo huo unachukuliwa kama moyo
wa Mawasiliano kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), hasa
katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na utakidhi mahitaji ya teknolojia ya
karne ya 21 kwa wateja wetu.
“Pia mfumo huu unalenga kutoa huduma kwa
haraka kwa wateja wetu na utatoa huduma nyingi na kwa urahisi ili kuyafikia
makundi mbalimbali ya wateja wake,” aliongeza.
Aliongeza pia wateja wa simu hizo watapata
huduma kwa mteja kwa njia ya data na sauti kupitia mfumo mpya unaojumuisha
malipo ya baada kwa ujumla.
Alisistiza kwamba mfumo huo utaleta uwazi
zaidi katika ulipaji wa malipo ya baada na kukidhi mahitaji ya makundi
mbalimbali na watu binafsi.
Naye Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam
Kaskazini wa Kituo cha Huduma kwa Mteja wa kampuni hiyo, Bw. Karim Bablia alisema
mfumo huo imesaidia kuingiza teknolojia mpya ya mawasiliamo simu za mezani na
mkononi ambayo haikuwepo Afrika Mashariki.
“Hii imesaidia huduma ya malipo ya baada
na inaambatana na punguzo na pia itasaidia wateja kupata taarifa kwa
wateja njia ya mtandao kupunguza malalamiko mbalimbali,”aliongeza Bw.Bablia.
Alisema hatahivyo itasaidia kupunguza
gharama za uendesjai kutokana na upatakanaji wa teknolojia hiyo mpya ambayo
hurahisisha mawasiliano.
Pia alisema miongoni mwa huduma
zinazoambatana na mfumo huo ni pamoja na kuondoa mfumo wa namna ya kupiga simu
kwa wateja wa malipo ya kabla ambao ulikuwa unausumbufu kwa wateja wa malipo
hayo.
Alisema kwa sasa kadi (Vocha) moja
itatumia kulipia huduma zote za malipo ya kabla ikilinganishwa na kadi mbili
zilizokuwa zikitumika hapo awali na pia kadi hiyo itatumika kulipia malipo ya
baada.
Pia wateja wataweza kuptaa huduma ya
taarifa binafsi kwa mteja kupitia mtandao kama kuangalia malipo ya baada au
bili kuongeza salio, kutoa taarifa za malalamiko na kununua huduma na kuhamisha
salio bila kizuizi.
Kampuni hiyo ni ya Serikali na inatoa
huduma ya mawasiliano na imejidhatiti kuzidi kuanzishaji bidhaa mpya zenye bei
nafuu,na wateja kuwa na uhakika wa kupata taarifa mbalimbali kupitia mtandao na
huduma za kibinafsi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment