Wednesday, March 27, 2013

Business environment set more improvement



By a Correspondent, Dar es Salaam

THE government through Tanzania Investment Centre (TIC) will continue improving the current business and investment environment to attract more local and foreign investments.

Minister of State in Prime Minister’s Office (Investment& Facilitation), Dr Mary Nagu, told a delegation of Chinese investors that Tanzania was creating a conducive environment that would stimulate business and investments growth in the country.

“We are fully committed to have conducive and enabling business environment that will enable us to widen up the base of more service provision and boost the economic growth,” Dr Nagu said during the dinner hosted in honour of visiting investors.

He said it was an undeniable fact that the government’s budget is not enough to meet requirements of every Tanzania of providing employment and good social service.

“It is our hope that if the business environment is improved more investors come forward and inject their capital into different sectors of economy hence bringing a multiplier effect to the country,” the minister said.

She said the delegation comprised  investors from 15 big companies  in China who were encouraged  the  recent visit of their president  Xi JinPing.

“While in Tanzania , the President of United Republic of  People’s of  China, Mr JinPing  directed Chinese investors to invest in Africa particularly in the country where there are abundant of investment opportunities,” she  noted.

The minister also took the splendid opportunity to invite them to seize the available investment opportunities and exploit services rendered by the investment centre.

Earlier, the  TIC acting Executive Director,  Mr Raymond Mbilinyi, said after meeting  the investors have shown interest to come and invest into different sectors of economy.

 “They met public and private companies where they shown interest to invest in education, electricity, infrastructure, agriculture and health,” Mr Mbilinyi explained.

According to Mr Mbilinyi, China is among the leading countries having more investments in Tanzania.

“We (TIC) have been a lot encouraged especially after our two presidents (Kikwete and Jin Ping) to show the way and commitment there the private sectors in both countries need fully utilize the opportunities.

Ends.

TPSF yapania kujenga uwezo kwa wanachama wake




Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (tpsf), Godfrey Simbeye ikisisitiza jambo wakati wa mkutano maalumu wa kuwajengea uwezo wanachama wa taasisi hiyo katika kanda ya kaskazini, juu ya umuhimu wa kongano (clusters) na jinsi ya kuimarisha mabaraza yao ya biashara ya wilaya na mikoa ili kuwa na sauti moja yenye nguvu kwa taasisi hiyo, mkutano huo ulifanyika jijini Arusha jana na kujumuisha mikoa ya Manyara, Kilimanjaro na Arusha.



Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (tpsf), Godfrey Simbeye ikisisitiza jambo wakati wa mkutano maalumu wa kuwajengea uwezo wanachama wa taasisi hiyo katika kanda ya kaskazini ,juu ya umuhimu wa kongano (clusters) na jinsi ya kuimarisha mabaraza yao ya biashara ya wilaya na mkoa ili kuwa na sauti moja yenye nguvu kwa taasisi hiyo, (kushoto) ni Mkurugenzi wa Bodi ya taasisi hiyo DKT. Gidion Kaunda. Mkutano huo ulifanyika jijini Arusha jana na kujumuisha mikoa ya Manyara, Kilimanjaro na Arusha.

Na Mwandishi Wetu, Arusha
Taasisi ya Sekta Binafsi nchini imesema itaendelea kuimarisha wanachama wake katika ngazi za kanda kwa kuwapa elimu ya biashara ili kukabiliana na soko la Afrika Mashariki linaloendelea kukua kwa kasi kwa sasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Bw. Godfrey Simbeye aliyasema hayo jijini Arusha muda mfupi mara baada ya kukutana na wanachama wa kanda ya kaskazini ambapo pamoja na mambo mengine wametakiwa kuimarisha vyama vyao vya biashara katika ngazi ya mikoa na wilaya.
“Napenda tuelewe kuwa wanachama walioko katika kanda ya kaskazini wako mipakani hivyo ni jukumu letu kutoa elimu ya kibiashara ya jinsi ya wao kuingia katika ushindani wa soko la Afrika Mashariki,” alisema Simbeye.
Alisisitiza kuwa kwa sasa kuna programu maalumu ya kutoa elimu ya kuendeleza wafanyabiashara ijulikanayo kama (Trade Mark East Afrika) inayoangalia fursa zilizopo katika mikoa ya kanda ya kaskazini ili wafanya biashara wa ukanda huo waweze kuchangamkia na kunufaika na fursa zilizopo.
Aliongeza kuwa TPSF kwa kushirikiana na TCCIA katika ngazi ya kanda wameanzisha program nyingine ya kuendeleza wajasiriamali wadogo waweze kuzalisha na kuuza zaidi.
“Katika kuhakikisha kuwa wanachama wa TPSF wanakuwa kitu kimoja na kujenga sauti moja yenye nguvu, wajasiriamali wadogo wanaangaliwa kwa ukaribu hasa kwa kuanzisha  program mbalimbali za kuwainua kiuchumi katika maeneo yao ya biashara waweze kuingia katika kundi la wafanyabiashara wa kati,” alisisitiza.
Alisema programu kama hizo ni njia tu ya kuelekea katika kuimarisha uchumi wa nchi kupitia wafanya biashara wadogo ambao wakiwezeshwa kielimu na kimtaji wataweza kuwa wafanyabiashara wakubwa hapo baadae.
Akizungumzia mabaraza ya wilaya na mikoa, Bw. Simbeye aliyataka kufanya kazi kwa ukaribu zaidi na taasisi hiyo ikiwa ni katika kujenga umoja na nguvu zaidi katika mikoa na wilaya.
Alisema kwa sasa mabaraza hayo yamekuwa kimya kutokana na kutokutana mara kwa mara na kujadili mustakabali wa masuala mbalimbali ya kibiashara katika mikoa na wilaya zao.
“Kikubwa ninachotaka kuwaambia viongozi katika mabaraza ya biashara ya mikoa na wilaya wafanye mikutano kama katiba inavyoelekeza, mabaraza haya hajakaa kwa muda mrefu hivyo ni wakati wao wa kukutana na kujadili matatizo yaliyopo katika maeneo yao,” alisema Mkurugenzi huyo.
Akizungumzia umuhimu wa mabaraza hayo kwa uchumi wa taifa Bw. Simbeye alisema mabaraza ya wilaya na mikoa ni muhimu sana si kwa uchumi wa mkoa bali kwa taifa na hii ni kutokana na kuhusisha pande zote mbili za sekta ya umma na binafs katika kukaa na kujadili maendeleo ya wilaya na mkoa kwa ujumla.
Mkutano huo wa kuimarisha sauti moja ya taasisi ya sekta binafsi nchini kwa kanda ya kaskazini umejumuisha mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro.
Wanachama wa taasisi hiyo walijadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na fursa mbalimbali za kiuchumi katika mikoa ya kanda hiyo pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Mwisho


Monday, March 18, 2013

Govt keen on creating conducive investment climate



The Minister of State, Prime Minister’s Office, Investment and Empowerment, Dr. Mary Nagu (second left) presenting a Tanzania Portland Cement Company (TPCC) certificate of incentive to the State Secretary for Foreign Affairs of Germany, Prof. Harald Braun (right) over the weekend in Dar es Salaam.  Others in the picture is the Germany’s State Secretary for Economy, Ms. Anne Ruth (second right); the TPCC Managing Director, Mr. Pascal Lessoine (third right) and the Acting Executive Director of Tanzania Investment Centre (TIC), Mr. Raymond Mbilinyi (left).

By a Correspondent, Dar es Salaam
The government of Tanzania has promised to continue supporting investors who facilitate growth of industrial activities in the country.
The assurance was given by the Acting Executive Director of Tanzania Investment Centre (TIC), Mr. Raymond Mbilinyi just after the handing over of a certificate of incentive to Tanzania Portland Cement Company (TPCC) that took place in Dar es Salaam over the weekend.
The certificate issued by TIC will facilitate the company invest more in the country and see it use more than Tshs 75 billion in its expansion endeavors.
TPCC Ltd is trading under Twiga Cement and Twiga Aggregates.  It is listed on the Dar es Salaam stock exchange where Heidelberg Cement Group of Germany holds 69.7 per cent of the shares.
As part of its expansion drive, Twiga has decided to extend its range of products for customer in Tanzania and in the coming months, construction companies operating in Tanzania will have an opportunity to buy aggregates for their projects from Twiga Aggregates.
“We will continue creating conducive environment to investors in Tanzania,” Mr. Mbilinyi said.
The Twiga cement expansion will see it add 700,000 tons of cement in production and enable it reach 2 million tons per annum.
Earlier, the Minister of State, Prime Minister’s Office, Investment and Empowerment, Dr. Mary Nagu who presented the certificate said it will help strengthening Twiga Cement and therefore the country’s construction industry.
“This will help you expand and therefore produce more cement and aggregates which are vital to construction industry, one of major drivers of our economy,” she said.
The Minister said that the government will continue play its role to reduce cost of doing business in the country for the benefit of investors and for the national development.
“We will make sure that investors get returns on their investments in this country and also expand the country’s tax base and create more employment opportunities,” she said.
On his part, the State Secretary for Foreign Affairs of Germany, Prof. Harald Braun who was present during the handing over of the certificate said that public private partnership (PPP) is very important for attaining sustainable development.
Talking on the diverse resources that Tanzania is endowed with he explained that it is PPP arrangement that can bring benefits out of those resources to people.
The last five years have seen TPCC invest Tshs 255 billion in its expansion drive.
Ends        

TPSF yahamasisha umoja sekta binafsi




Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bw. Geofey Simbeye akisisitiza jambo kwa wanachama wa taasisi hiyo wa kanda ya ziwa katika mkutano maalumu wa uelimishaji na uhamasishaji wa muundo wa uwakilishi katika kongano ( clusters).  Kulia ni Mkurugenzi wa Bodi ya TPSF Bw. Gideon Kaunda.  Mkutano huo ulifanyika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.



Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Bw. Geofey Simbeye akizungumza na wanachama wa taasisi hiyo kutoka kanda ya ziwa katika mkutano maalumu wa uelimishaji na uhamasishaji wa muundo wa uwakilishi katika kongano( clusters) mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.


Na Mwandishi Wetu, Mwanza
Mchakato wa kuwa na sauti moja, imara na yenye nguvu nchini kwa sekta binafsi unaendelea vizuri baada ya kuanza mikutano ya uhamasishaji ya kikanda huku wanachama wa taasisi hiyo wakihimizwa kuwa kitu kimoja ili kuingia katika ushindani wa soko la Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF), Bw. Geofrey Simbeye, alisema mchakato huo ulioanza mwaka 2011 lengo lake ni kuweka mazingira bora na wezeshi kwa wanachama wake katika kuongeza kasi ya uanzishwaji wa makampuni na viwanda kwa ajili ya kuongeza ajira na kuinua uchumi wa nchi.
“Pia kuishawishi serikali kuondoa baadhi ya vikwazo katika ufanyaji biashara ndani na nje ya nchi,” alisema Bw. Simbeye katika mkutano wa kanda ya ziwa ulioshirikisha wanachama hao jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Alisema TPSF inataka wanachama wake wafahamiane katika ufanyaji biashara hasa katika mikoa iliyopo katika kanda moja pia kujenga kongano (clusters) imara zitakazoweza kuwaunganisha katika sekta mbalimbali za kiuchumi.
Aliongeza kuwa mikutano hiyo ya kanda itahamasisha wawekezaji waliopo katika mikoa husika kuwekeza kutokana na fursa zilizopo katika mikoa hiyo.
 Akizungumzia kanda ya ziwa Mkurugenzi huyo alisema kanda ya ziwa ni moja ya kanda zenye fursa nyingi za uwekezaji hapa nchini, hivyo ni changamoto kwa wanachama wa TPSF katika mikoa hiyo kuungana ili kuisaidia serikali katika kuweka mazingira bora na wezeshi ya kufanya biashara na uwekezaji.
“Serikali inaitegemea sana sekta binafsi katika kujenga uchumi wa nchi, kwa hiyo napenda niseme ya kwamba watu wa kanda ya ziwa wana nafasi kubwa ya kuisaidia serikali katika kutekeleza jukumu hilo,”aliongeza Mkurugenzi huyo.
Alisisitiza kuwa baada ya mikutano hiyo ya kanda wanaamini watapata wawakilishi watakaoingia katika bodi ya TPSF ambao watawakilisha kanda nane zilizoanishwa katika mtindo wa kongano na hivyo kuwa na sauti moja itakayounganisha wanachama wote nchi nzima.
“Ukishakuwa na sauti moja katika jambo lolote lile lazima utafanikiwa, tunaomba serikali iweze kuangalia uwezekano wa kutupunguzia kodi kwa sisi watu wa sekta binafsi,” alisisitiza Bw. Simbeye.
Aidha Bw. Simbeye aligusia suala la uwajibikaji kwa wananchama wa taasisi hiyo katika kuchangia mawazo yao ili kuleta mabadiliko ya kiuchumi si kwa TPSF tu bali na sekta nyingine za kiuchumi.
“Mimi siku zote nimekuwa nikihimiza viongozi wa vyama vya biashara vya mikoa ambavyo ni wanachama wa TPSF kuwa kitu kimoja ili serikali iendelee kuiamini sekta yetu katika kuendelea kubadili uchumi wa nchi hii,” aliongeza.
Mkutano huo wa siku moja uliofanyika jijini Mwanza ulikuwa na lengo la kuelimisha na kuhamasisha muundo wa uwakilishi katika kongano (clusters) na kuhusisha mikoa ya  Kagera, Mara, Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza, ambayo inaunganisha kanda ya ziwa.
Mwisho  

Wednesday, March 13, 2013

Uhusiano wa wazazi, watoto muhimu kwa maendeleo shuleni



Mkuu wa Shule ya Ndetembia Matemu iliyo katika eneo la Kihonda katika Manispaa ya Morogoro Mkoani Morogoro, Ms. Christina Gumbo akisisitiza jambo wakati akielezea maendeleo ya elimu katika shule yake pamoja na maoni yake jinsi ya kuimarisha sekta hiyo hapa nchini jana mjini Morogoro.

The Head Teacher of Ndetembia Matemu primary school in Kihonda, Morogoro region, Ms. Christina Gumbo stresses something when talking to journalists yesterday in Morogoro on matters related to education development in the country.

Na Mwandishi wetu, Morogoro

Wakati wadau wa elimu nchini wakilalamikia kushuka kwa kiwango cha elimu na ufaulu mdogo katika mitihani ya kitaifa, wazazi na walezi wametakiwa kuwa karibu na watoto wao ili kuleta mabadiliko haraka katika sekta hiyo muhimu kwa maendeleo.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Ndetembia Matemu iliyopo katika eneo la Kihonda katika manispaa ya Morogoro Mkoani Morogoro, Bi. Christina Gumbo alitoa wito huo kwa waandishi wa habari wakati akitoa maoni yake kuhusiana na maendeleo ya elimu katika shule yake na hapa nchini kwa ujumla.

“Sekta binafsi inatakiwa ijikite zaidi katika kuwekeza zaidi kwenye elimu, lakini na wazazi wahimize watoto wao kukazania elimu kwa kuwa ndio itakayowasaidia kubadilisha hali ya uchumi katika nchi,” alisema Mwalimu Gumbo.

Aliongeza kuwa msingi bora wa kumlea mototo unaanzia nyambani, hivyo ni vema wazazi wakawakumbusha kila mara watoto umuhimu wa elimu na mustakabali wa maisha yao ya baadae ili waweze kuzingatia kile wanachopewa na walimu wawapo masomoni.

“Mwalimu ni mzazi wa pili awapo shuleni, sisi pia tunafundisha kama wazazi tofauti ni kwamba hapa shuleni masomo na nidhamu ndio yanazingatiwa kwa umakini wa hali ya juu,” alisisitiza mkuu huyo wa shule.

Akizungumzia lengo la kuanzishwa kwa shule hiyo alisema wameitikia sera ya serikali ya kuwekeza katika elimu kutokana na uhaba uliopo wa shule za msingi na sekondari katika katika halmashauri na manispaa mbalimbali hapa nchini.

“Siku zote serikali imekuwa ikihimiza wadau mbalimbali kujenga shule bora na zenye kiwango ili kuongeza fursa za masomo hapa nchini,” alisema.

Matokeo ya kidato cha nne ya hivi karibuni yamelalamikiwa sana na wadau mbalimbali hapa nchini wakidai ni kutokana na nidhamu isiyoridhisha miongoni mwa wanafunzi, wazazi kutokua karibu na watoto miongoni mwa sababu nyingine.

Shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2010 ina wanafunzi 177 kuanzia chekechea hadi darasa la nne.

“Ni lengo letu kutayarisha wanafunzi watakaokua na uwezo na kufanya vyema katika masomo yao,” alisema.

Mwisho

Sunday, March 10, 2013

Serikali kuimarisha ushirikiano na China kupitia uwekezaji, biashara



Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Raymond Mbilinyi (kulia) akimsikiliza Kaimu Kamishna wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Bw. Suleiman Kova (kushoto) wakati wa mkutano wa maswala ya usalama na uwekezaji mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.   




Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Raymond Mbilinyi (kulia) akimsikiliza Kaimu Kamishna wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Bw. Suleiman Kova (katikati) wakati wa mkutano wa maswala ya usalama na uwekezaji mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  Kushoto ni Mwakilishi Mkuu wa maswala ya uchumi na biashara wa China nchini Tanzania, Bw. Lin Zhiyong.

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Serikali imesema itahakikisha inaimarisha uhusiano wake na wawekezaji toka China kwa manufaa ya nchi zote mbili.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Raymond Mbilinyi amesema katika mkutano wa maswala ya usalama na uwekezaji mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam kuwa serikali itatumia uwekezaji na biashara baina ya nchi hizo kama moja ya njia za kuimarisha uhusiano wa muda mrefu kati ya mataifa hayo.
Mkutano huo uliolenga wawekezaji wa Kichina wanaoishi Dar es Salaam ulihudhuriwa na maafisa mbalimbali wa serikali kutoka polisi, TIC, uhamiaji na idara ya kazi.
“Maeneo haya ya uwekezaji na biashara yana uwezo wa kuimarisha uhusiano wetu kwa kiwango kikubwa,” alisema.
Mkutano huo uliandaliwa kwa ushirikiano kati ya Kituo cha Biashara cha China nchini Tanzania (CBCT) na TIC kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya CBCT na idara mbalimbali za serikali ya Tanzania.
Bw. Mbilinyi alimshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa juhudi zake katika kuimarisha uhusiano na nchi hiyo ambayo ni miongoni mwa zenye uchumi mkubwa kabisa duniani na kuwataka wawekezaji hao kulenga sekta zinazozalisha ajira kwa wingi kama vile uzalishaji na ujenzi.
“Tunapenda kusisitiza ushirikiano na wawekezaji wa ndani ili kuleta mafanikio makubwa zaidi,” alisema Bw. Mbilinyi na kuongeza kuwa kama wawekezaji hao watafuata sheria na taratibu za nchi watafanikiwa katika malengo yao.
Mwenyekiti wa CBCT, Bw. Janson Huang alisema siku zote nchi ya China itaheshimu uhusiano wa siku nyingi kati ya pande hizo na kwamba wataonyesha kwa vitendo heshima hiyo kwa kuajiri wafanyakazi wazalendo katika kampuni zao hapa nchini na kujihusisha katika kutoa misaada mbalimbali ya kiutu hapa nchini.
Bw. Huang alisema kuwa usalama ni swala muhimu sana katika kuendesha biashara na akapendekeza kuanzishwa kwa kituo cha ushirikiano kati ya polisi na jumuia ya wachina hapa nchini kushughulikia maswala ya kiusalama ya kila siku yanayowahusu.
Pia alitoa ombi kwa serikali ya Tanzania kuangalia jinsi ya kurahisisha taratibu nzima za kutoa vibali mbalimbali kwa wawekezaji hao ili kuimarisha zaidi ushirikiano.
Kwa upande wake, Kaimu Kamishna wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Bw. Suleiman Kova alisema kwamba kikosi chake kiko tayari kulinda wawekezaji na mali zao ili kuhakikisha mazingira ya uwekezaji yanaboreka zaidi na hivyo kukuza uchumi wa nchi.
Hata hivyo, alitoa angalizo kuwa ni lazima wawekezaji hao kufuata sheria na taratibu za nchi na kwamba kamwe wasiwe chanzo cha matatizo.
“Tutazidi kushirikiana na idara nyingine za serikali kuhakikisha kuwa wawekezaji wanakua salama,” alisema.
Uhusiano kati ya Tanzania na China ni wa kihistoria na uliasisiwa na viongozi, Mwenyekiti Mao Zedong wa China na Rais Julius Nyerere na kudumu zaidi ya miaka hamsini hadi sasa.
China imekua ikijihusisha na miradi mbalimbali hapa nchini.
Takwimu zinaonyesha kuwa uwekezaji wa China hapa nchini umekua thabiti katika miaka ya hivi karibuni, nchi hiyo ikiwekeza miradi yenye thamani ya zaidi USD bilioni moja kupitia kampuni zaidi ya 300 na kutengeneza ajira zaidi ya 80,000 kwa watanzania.
Hivi karibuni, nchi hiyo iliipatia Tanzania mkopo wa dola za kimarekani 1.01 bilioni kugharamia ujenzi wa bomba la gesi lenye urefu wa kilometa 522 kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam kwa riba ya asilimia 3 tu.
Mradi huo unatarajiwa kumaliza tatizo sugu la umeme hapa nchini na hivyo kuimarisha uchumi.
Mwisho 


PASS kufufua miradi ya umwagiliaji nchini, kusaidia wakulima wadogo



Mjumbe wa Bodi ya wadhamini ya Asasi ya Kusaidia Uwekezaji Kwenye Kilimo (PASS Trust), Bw. Salum Diwani (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi hiyo Bw. Iddy Lujina muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao cha bodi hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.




Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Asasi ya Kusaidia Uwekezaji Kwenye Kilimo (PASS) imetenga shilingi bilioni 4 kwa ajili ya kutoa huduma mpya ya mikopo ya Karadha ili kusaidia kufufua miradi ya umwagiliaji na wakulima wadogo wadogo hapa nchini kwa mwaka huu.
Kwa kuanzia, mikopo hiyo ya karadha itaanza kusaidia juhudi za kufufua mradi wa umwagiliaji Moshi katika mazao ya mpunga na mahindi kwa kutoa Tshs 400 milioni mwezi ujao ili kupata matrekata na vifaa vya kuvunia mazao.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini PASS, Profesa Andrew Temu aliwaambia hayo waandishi wa habari mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam mara baada ya kikao cha bodi ya wakurugenzi wa asasi hiyo.
“Kikao chetu cha bodi kimeamua kuanzisha mikopo ya karadha ambayo imeanza na ukanda wa kaskazini wa nchi ambapo kupitia fedha hiyo mradi huo utapata matrekta nane na vivunio sita,” alisema.
“Huu ni mfumo wa karadha ambapo wakulima baada ya kurejesha mikopo yao vifaa hivyo vitakuwa vya kwao,” alisema na kuongeza kuwa mikopo hiyo ya vifaa vya kilimo itasaidia sana pia na wakulima wadogo wanaoishi katika na pembezoni mwa mashamba hayo makubwa ya umwagiliaji maana wao hawana uwezo wa kupata vifaa hivyo.
Alisema awamu ya pili itahusisha kiasi cha Tshs 800 milioni katika kanda hiyo.
Alisema baada ya ukanda huo asasi hiyo italenga pia kanda nyingine kama vile mradi wa umwagiliaji wa Dakawa, Morogoro kwa kilimo cha mpunga; Mradi wa umwagiliaji Madibira, Iringa na maeneo mengine.
Alisema asasi yao sasa itafanya kazi pia na benki za kijamii ikiwemo ya Kilimanjaro Community Bank LTD, Pride na nyingine mkoani Arusha ili kuwafikia kwa karibu wakulima wadogo.  
Pia asasi hiyo inashirikiana na benki nyingine kama CRDB, Exim Bank, TIB, NMB na NBC.
Alisema asasi yao inaunga mkono juhudi za serikali na mkakati wake wa kuendeleza kilimo katika ukanda wa kusini mwa Tanzania (SAGCOT) na kusema kwamba ili mpango huu uweze kufanikiwa kwa kiwango cha juu, unahitaji huduma za kibenki.
Mkurugenzi Mtendaji wa PASS, Bw. Iddy Lujina alisema kilimo cha Tanzania bado kipo chini na kinahitaji huduma za kibenki kufikia kilimo cha kisasa.
“Tumeshakamilisha kufanya maboresho kwenye tawi la Moshi na tunatarajia kufungua tawi la Mtwara ili lihudumie Lindi na Mtwara kwa ajili ya kusogeza huduma kwa jamii,” alisema na kuongeza kuwa kwa  sasa wanatafuta eneo kufungua tawi Kigoma ili kuhudumia pia mkoa wa Tabora.
Alisema baada ya kufungua matawi hayo watakuwa na tawi la Mwanza, Moshi, Morogoro, Dar es Salaam, Mbeya, Mtwara na Kigoma kwa lengo la kusaidia upatakanaji wa huduma za mikopo katika kilimo katika kanda zote hapa nchini.
Kupitia huduma zake, mwaka 2011 PASS ilisaidia wakulima 11,000 kupata mikopo yenye thamani ya Tshs 22 bilioni kutoka kwenye benki mbalimbali na mikopo hiyo ilipanda hadi kufikia Tshs 30 bilioni mwaka jana.

Hadi sasa, taasisi hiyo ina matawi katika mikoa ya Morogoro, Mbeya, Dar es Salaam, Mwanza, Moshi na Mtwara.

Katika miaka kumi iliyopita, PASS imeweza kusaidia wakulima zaidi ya 100,000 kupata mikopo na katika mpango wake mpya wa miaka mitano inatarajia kusaidia wakulima zaidi ya 300,000 kuweza kupata mikopo yenye thamani ya Tshs 290 bilioni.

Mwisho