Wednesday, March 4, 2015

Kamati ya Bunge TAMISEMI yataka mradi mabasi yaendayo kasi uanze

Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya serikali za mitaa na tawala za mikoa (Tamisemi) Mh. Hamis Kigwangala (kushoto) akisikializa maelezo ya Meneja Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka kutoka TANROADS Mhandisi Elibariki Mmari wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka, (kulia) ni Mtendaji Mkuu wa DART Asteria Mlambo (wa pili) ni Mhandisi Athuman Mfutakamba mbunge wa jimbo la Igalua na mjumbe wa kamati hiyo.
Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya serikali za mitaa na tawala za mikoa (Tamisemi) Mh. Hamis Kigwangala (wa pili kulia) akimweleza jambo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI Hawa Ghasia wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa mabasi yaendayo haraka, (kulia) ni Mjumbe wa kamati hiyo Moses Machali (wa pili kushoto)  ni Naibu waziri TAMISEMI Kasim Majaliwa.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka ( DART) Asteria Mlambo (kulia) akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya serikali za mitaa na tawala za mikoa (Tamisemi) Mh. Hamis Kigwangala (wa pili kulia)  wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa mabasi yaendayo haraka, (wa pili kulia) ni Waziri wa nchi – TAMISEMI, Mh. Hawa Ghasia, (kulia) ni Mhandisi Athuman Mfutakamba mbunge wa jimbo la Igalua na mjumbe wa kamati hiyo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka ( DART) Asteria Mlambo (kushoto) akimweleza jambo Waziri wa nchi – TAMISEMI, Mh. Hawa Ghasia (katikati)   wakati kamati ya bunge ya tawala za mikoa na serikali za mitaa ( TAMISEMI) ilipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa mabasi yaendayo haraka, (kulia) ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh. Hamis Kigwangala.
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Kamati ya Bunge Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imetoa muda wa wiki mbili  kwa Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) na Wakala wa Barabara (TANROAD) kutoa taarifa ya inayoeleza muda halisi wa kuanza kwa mabasi ya mradi huo katika kipindi cha mpito.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge, Bw. Hamis Kigwangala alitoa maelekezo hayo jana jijini Dar es Salaam wakati kamati yake ilipokuwa ikipokea taarifa ya utekelezaji wa maradi huo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia DART na TANROADS.

“Kipindi cha mpito cha mradi huu kilikuwa kianze mwezi April mwaka huu lakini hadi sasa maandalizi yake bado hayakamilika,”alisema.

Alisema kutokana na hali hiyo kamati imetoa siku 14 kuanzia sasa waandae taarifa inayoonyesha  kukamilika kwa mandalizi hayo ikiwemo kusaini kwa mikataba na mtoa huduma na kuikabidhi taarifa hiyo.

“Tunahitaji kuona mabasi ya kipindi  cha mpito yanaanza kufanya kazi  katika kipindi cha miezi miwili kuanzia sasa,” alisema.

Alifafanua kwamba mradi huo ni muhimu kwa vile utaokoa  Tshs 4.5 bilioni kwa siku zinazopotea katika jiji la Dar es Salaam kutokana na msongamano wa magari.


Pia aliitaka TAMISEMI kwa kushirikiana na mamlaka nyingine kuhakikisha inawaondoa wafanyabiashara wanaofanya biashara zao katika miundombinu ya mradi huo.

No comments: