Monday, March 9, 2015

TPA yawahakikishia wadau wake ushirikiano zaidi

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) Bw. Awadh Massawe (kushoto) akisisitiza jambo kwenye mkutano uliohusisha mamlaka hiyo na wadau wake mbalimbali uliokuwa na lengo la kujenga mahusiano ya karibu kati yao ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi.  Mkutano huo ulifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) Bw. Awadh Massawe akisisitiza jambo kwenye mkutano uliohusisha mamlaka hiyo na wadau wake mbalimbali (hawako pichani) uliokuwa na lengo la kujenga mahusiano ya karibu kati yao ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi.  Mkutano huo ulifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Wadau wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) wakimsikiliza kwa makini Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Bw. Awadh Massawe kwenye mkutano uliohusisha mamlaka hiyo na wadau wake mbalimbali uliokuwa na lengo la kujenga mahusiano ya karibu kati yao ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi.  Mkutano huo ulifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) Bw. Awadh Massawe (aliyesimama) akisisitiza jambo kwenye mkutano uliohusisha mamlaka hiyo na wadau wake mbalimbali uliokuwa na lengo la kujenga mahusiano ya karibu kati yao ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi.  Mkutano huo ulifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) Bw. Awadh Massawe (kushoto) akibadilishana mawazo na wadau wa mamlaka hiyo, Bw. Elias Lukumay (katikati) na Bw. Rahim Dossa mara baada ya kumalizika mkutano uliohusisha mamlaka hiyo na wadau wake mbalimbali uliokuwa na lengo la kujenga mahusiano ya karibu kati yao ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi.  Mkutano huo ulifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Mamlaka ya Usimamizi Bandari Tanzania (TPA) imeelezea nia ya kushirikiana zaidi na wadau wake katika kuhakikisha huduma za bandari nchini zinazidi kuimarika na kuchangia zaidi pato la taifa.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Awadh Massawe amesema muda umefika wa kuwa na mtazamo mpya wa ushirikiano kati ya bandari na wadau wake toka sekta za umma na binafsi ili kuongeza ufanisi.

Akiongea katika kikao na wadau mbalimbali wa mamlaka hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Bw. Massawe alisema kikao hicho kilikuwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Waziri wa Uchukuzi, Bw. Samuel Sitta alipokutana na bodi ya mamlaka hiyo hivi karibuni.

Kati ya mambo mengine, Waziri Sitta aliiagiza bodi hiyo kuhakikisha kuwa mahusiano na wadau mbalimbali wa bandari yanaimarishwa.

“Bandari inaweza kufanya vyema zaidi kama tutashirikiana vyema na wadau wetu upande wa sekta binafsi,” alisema Bw. Massawe.


Aliwaambia waandishi wa habari kuwa ni kwa kupitia ushirikiano na kufanya kazi kwa karibu zaidi na sekta binafsi na wadau mbalimbali ndipo bandari za Tanzania hasa ya Dar es Salaam zitakapoweza kufanya vyema katika kipindi hiki cha ushindani mkubwa na bandari nyingine katika eneo hili la Afrika.

No comments: