Monday, March 9, 2015

Wahudumu wa bar 700 watunukiwa vyeti vya kimataifa vya Master Academy (MBA)

Mkuu wa Masoko na Vinywaji Vikali wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Bw. Stanley Samtu akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti wahitimu wa mafunzo ya kimataifa ya Diageo Master Academy   (MBA) yaliyoandaliwa kwa ajili ya kuwapa wahudumu hao ujuzi wa kufanya kazi kwa weledi, katikati ni Meneja Chapa wa Vinywaji Vikali wa kampuni hiyo, Bw.Shomari Shomari na wakwanza kulia ni Mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka Afrika Kusini,Bw. Mthokizisi Elvis.
Meneja  Biashara Mipango (Commercial Planning and Activation), wa  Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) ,Bw. Denis Tairo akimkabidhi cheti cha mafunzo ya uhudumu wa  baa, Bi. Betilda Miruko baada ya kuhitimu mafunzo ya kimataifa ya ‘ Diageo Master Academy’   (MBA) yaliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya kuwapa wahudumu hao ilikuongeza  ujuzi wa kufanya kazi kwa weledi,Kulia ni Meneja Chapa wa Vinywaji Vikali wa kampuni hiyo,Bw.Shomari Shomari,wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa Masoko na Vinywaji Vikali,Bw. Stanley Samtu na kulia ni Maneja wa Mahesabu wa kampuni hiyo,Bw. Francis Tibaikana.
Na Mwandishi wetu,Dar es Salaam
Kampuni ya Bia ya Serengeti imewatunuku vyeti wahudumu wa bar 700 walioshiriki mafunzo ya kimataifa ya Diageo Master Academy   (MBA) yaliyoandaliwa kwa ajili ya kuwapa wahudumu hao ujuzi wa kufanya kazi kwa weledi.

Akitunuku vyeti hivyo kwa wahitimu hao jijini DSar es salaam jana,Mkuu wa Masoko wa Vinywaji Vikali (Head of Marketing Sprit), Bw. Stanley Samtu,mafunzo hayo yatawawezesha wahitimu hao kushiriki shindano la kitaifa na la kimataifa la Diaego Master Bar Academy .

“Tumewatunuku vyeti vya kimataifa vya MBA wahudumu wa bar kutoka mikoa kumi nchini baada ya kuhitimu mafunzo ya mwezi mmoja,”alisema.

Alisema mafunzo hayo yamewapatia ujuzi wa kuhudumia wateja, kuchangana bia, kujua wajibu wao na aina ya viunywaji vikiwemo vya Barleys,Gordons,Grants,  John Walker, Guiness, Smirnoff na na jamii zote za bia za Serengeti.

Alisema mafunzo hayo ya kimataifa kwa Afrika yalianza kutolewa  Februari 7, 2015 na kukamilika tarehe 7 Machi 2015 na wakufunzi  kutoka Afrika Kusini.
“Mafunzo hayo yalifanyika katika mikoa  ya Dodoma, Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Morogoro, na Mbeya,”alisema.

No comments: