Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia
Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu
(kulia) akimkaribisha Meya wa Mji wa
Vallejo uliopo Jimbo la California nchini
Marekani, Bw. OSby Davis (kushoto) katika
mji wa Bagamoyo ambapo meya huyo
aliambatana na wafanyabiashara wa mji
wake kuja kuangalia fursa za biashara za
mji wa Bagamoyo, katikati ni Mwenyekiti
wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri
ya Bagamoyo, Bw. Shukuru Mboto.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia
Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu( kushoto) akibadilishana mawazo na Meya wa Mji wa Vallejo
uliopo Jimbo la California nchini Marekani, Bw. OSby Davis (kulia) mara tu baada ya meya huyo na wafanyabiashara wa mji huo kuwasili katika mji wa Bagamoyo jana.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu( kushoto) akifungua mkutano uliowashirikisha wafanyabiashara wa mji wa Vallejo
uliopo Jimbo la Carifonia nchini Marekani
na mji wa Bagamoyo, wapili kushoto ni
Meya wa Mji wa Vallejo, Jimbo la California Marekani, Bw. OSby Davis, kulia ni Mkuu wa Mkoa
wa Pwani, Bi. Mwantumu Mahiza na wapili kulia ni Meya wa Jiji la
Dar es Salaam Dkt. Didas Masaburi.
Wafanyabiashara wa Mji wa Vallejo uliopo Jimbo la California nchini
Marekani na mji wa Bagamoyo wakifuatilia kwa umakini mada iliyokuwa ikitolewa na kituo cha uwekezaji nchini (TIC) kuhusu fursa za
uwekezaji na biashara zinazopatikana katika mji wa Bagamoyo na Tanzania kwa
ujumla.
Wednesday, February 26, 2014
Monday, February 24, 2014
TNBC yashauri baraza la biashara Manyara kuchapa kazi zaidi
Mwandishi wetu, Manyara
Wajumbe wa Baraza la Biashara
la Mkoa wa Manyara wameshauriwa kuchapa kazi kwa bidii na kuongeza ushirikiano miongoni
mwao ili kuzidi kusaidia kujenga mazingira bora ya biashara na uwekezaji mkoani
humo kwa maendeleo ya mkoa na nchi kwa ujumla.
Katibu Mtendaji wa Baraza la
Taifa la Biashara (TNBC), Bw. Raymond Mbilinyi aliwaambia waandishi wa habari mkoani
humo mwishoni mwa wiki kuwa wajumbe hawana budi kuhakikisha wanafanya kazi kwa
ushirikiano zaid ili kukuza shughuli za biashara na uchumi.
“Napongeza baraza hili ambalo
limejumuisha wajumbe kutoka sekta ya umma na binafisi kwa kuonesha mwamko mkubwa
wa kufanya kazi,” alisema.
Alisema biashara na uwekezaji
katika mazingira ya sasa unategemea sana ushirikiano wa sekta ya umma na
binafsi kukaa pamoja na kujadili namna ya kuendeleza biashara na uwekezaji.
Alisema wajumbe wa baraza wanatakiwa kujadili kwa uwazi vikwazo na njia
ya kuyatatua na pale inaposhindikana yapelekwe kupatiwa suluhisho katika ngazi
ya taifa.
Alisema Desemba mwaka 2013
ulifanyika mkutano wa saba wa Baraza la Biashara la Taifa, chini ya Uwenyekiti
wa Rais Jakaya Kikwete na ajenda zilikuwa tatu ikiwemo watanzania kushiriki
katika uchumi, Matokeo Makubwa Sasa na kuboresha mazingira ya biashara.
Alisema ajenda hizo zinatakiwa
kufanyiwa kazi katika ngazi ya mkoa ili kupata ufanisi zaidi.
“Nitafurahi kuona baraza la
mkoa huu mkiendeleza hili kwa nguvu ili kufikia malengo yanayokusudiwa,”aliongeza
kusema Bw. Mbilinyi.
Akifafanua zaidi alisema ngazi
ya mkoa na wilaya zikiweka mazingira bora ya biashara itasaidia wafanyabiashara
kushiriki vema na kuwa hayo yote yanategemea zaidi wajumbe hao wa baraza.
Kwa upande wake, Mwenyekiti
wa Baraza la Biashara la Mkoa wa Manyara, ambaye pia Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Elaston
Mbwilo alisema sekta ya umma itahakikisha inashirikiana vizuri na sekta binafsi
kupitia baraza hilo.
“Sekta ya umma itafanya kazi
kulingana na jinsi tunavyojadili hapa katika kukuza biashara na uwekezaji,”
alisema Bw. Mbwilo.
Alisema mkutano huo ulikuwa
ni fursa kubwa kwao kuzungumzia maswala yanayolenga kujenga biashara na
uwekezaji wa mkoa wao.
Pia alitoa wito kwa baraza
hilo kuziunganisha sekta ndogo za ufugaji na Kilimo ambazo ndizo shughuli kuu
za mkoa huo lakini zimekuwa hazina mahusiano mazuri.
Aliagiza kufanyika kongamano
ambalo litawaunganisha wafugaji kwa kuwa hawana umoja kama ilivyo kwa wakulima.
Mwisho
TTCL yaahidi makubwa mradi wa mawasiliano vijijini
Afisa Mkuu
wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Peter Ngota
(kulia) pamoja na Afisa Mtendaji mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF),
Bw. Peter Ulanga wakitia saini mkataba wa mradi wa kutoa huduma za mawasiliano
vijijini wenye thamani ya Tshs 9.8 bilioni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa
wiki. Waliosimama ni Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Prof. John Nkoma (kushoto),
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa (katikati)
na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dr. John Mngodo.
Na
Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) imeahidi kutekeleza kwa ufanisi na kwa wakati zabuni iliyoshinda ya mradi wa kutoa huduma za mawasiliano vijijini.
Ahadi hiyo imetolewa na Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Kampuni hiyo, Bw. Peter Ngota alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kampuni hiyo kutiliana saini na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
TTCL inatekeleza mradi huo wenye thamani ya Tshs 9.8 bilioni baada ya kushinda zabuni hiyo.
Ushindi huo unamaanisha kuwa baada ya kukamilisha mradi huo, TTCL itakuwa na uwezo wa kutoa huduma za mawasiliano katika kata 33 zenye jumla ya vijiji 202 vyenye jumla ya wakazi zaidi ya 300,000 katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
“Tutafanya kwa ubora zaidi katika awamu hii kwa maana tuna uzoefu wa kina kwani kwa sasa tunao wataalamu wenye ujuzi na uzoefu wa kutosha kusimamia miradi ya aina hii,” alisema Bw. Ngota aliyekuwa akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Dkt. Kamugisha Kazaura.
Bw. Ngota alisema kampuni hiyo ni muhimili wa mawasiliano Tanzania kwa zaidi ya miaka hamsini sasa katika kutoa huduma za mawasiliano hivyo hawana shaka yoyote katika kutekeleza mradi huo.
Katika awamu ya kwanza yenye kata 20 kampuni hiyo pamoja na kampuni nyingine za simu hapa nchini ilishinda zabuni yenye thamani ya Tshs 3.4 bilioni ambayo inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu.
Bw. Ngota aliiomba Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia pamoja na UCSAF na wadau wengine kuendelea kushirikiana katika kuleta mapinduzi ya mawasiliano bora kwa wananchi wengi ili kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Awali, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa alisema serikali inatambua umuhimu wa watoa huduma za mawasiliano katika kupeleka mawasiliano sehemu zenye mawasiliano hafifu.
“Upelekwaji wa mawasiliano umeendelea kuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi wa kijamii katika maeneo hayo,” alisema.
Alisema ni shauku ya serikali kuona kuwa huduma zote wanazofurahia watu wa mijini kutokana na matumizi ya TEHAMA zinawafikia pia watu wa vijijini ifikapo mwaka 2015.
Afisa Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Injinia Peter Ulanga alisema mfuko wake umedhamiria kuona maeneo mengi zaidi vijijini yanafikiwa na huduma za mawasiliano.
“Hii ni kwa mujibu wa dira ya maendeleo ya serikali na mkakati huu utasaidia kufikia maendeleo endelevu hapa nchini,” alisema.
Vijiji husika vya mradi huu viko katika mikoa 16 ambayo ni Arusha, Tabora, Iringa, Kagera, Manyara, Dodoma, Lindi, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Pwani, Ruvuma, Shinyanga, Singida na Tanga.
Mradi huu ulifadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia UCSAF ambao upo chini ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia umepangwa kumalizika ndani ya kipindi cha miezi nane kuanzia Februari 20 mwaka huu. TTCL pia itagharamia kiasi cha pesa katika mradi huo.
Kwa kuanzia, huduma zitakazotolewa ni zile za msingi kama huduma za ujumbe mfupi, mtandao wa intanenti kupitia simu za mkononi na za mezani zisizotumia waya.

Subscribe to:
Posts (Atom)