Mkuu wa Shughuli za Biashara za Kibenki wa Benki ya Afrika Tanzania, Bw.Wasia Mushi (kushoto) akiongea na wagonjwa wa hospitali ya Walemavu ya CCBRT ya jijini Dar es Salaam Jumatatu ya Pasaka. Wafanyakazi wa benki hiyo waliungana na wagonjwa katika hospitali hiyo na kula chakula cha mchana pamoja katika sikukuu hiyo.
Mkuu wa Shughuli za Biashara za
Kibenki wa Benki ya Afrika Tanzania, Bw.Wasia Mushi (kushoto) akigawa chakula
kwa wagonjwa wa hospitali ya Walemavu ya CCBRT ya jijini Dar es Salaam Jumatatu
ya Pasaka. Wafanyakazi wa benki hiyo
waliungana na wagonjwa katika hospitali hiyo na kula chakula cha mchana pamoja
katika sikukuu hiyo.
Mkuu wa Shughuli za Biashara za Kibenki wa Benki ya Afrika Tanzania, Bw.Wasia Mushi (kulia) akigawa zawadi kwa wagonjwa wa hospitali ya Walemavu ya CCBRT ya jijini Dar es Salaam Jumatatu ya Pasaka. Wafanyakazi wa benki hiyo waliungana na wagonjwa katika hospitali hiyo na kula chakula cha mchana pamoja katika sikukuu hiyo.
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Kama moja ya sehemu ya huduma zake
kwa jamii, Benki ya Afrika Tanzania imeshiriki chakula cha mchana pamoja na
wagonjwa wa matatizo mbalimbali wa hospitali ya CCBRT.
Chakula hicho kiliandaliwa kwa ajili
ya maadhimisho ya sikuku ya Pasaka ambayo wakrito wote duniani husherehekea kufufuka kwa Yesu Kristo siku ya
Jumatatu ya Pasaka jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Shughuli za Kibenki, Bw.
Wasia Mushi alisema kila mwaka wafanyakazi wa benki yao hujumuika na wagonjwa
wa hospitali hiyo kwa ajili ya kuwafariji katika kipindi ambacho wanapata
matibabu.
“Tumejumuika na wenzetu ambao wana matatizo
mbalimbali kwa kuwaandalia chakula ili nao wajisikie vizuri katika sikukuu hii
ya Pasaka…ni moja sehemu ya huduma zetu kwa jamii,” alisema Bw. Mushi.
Alisema pia wao kama benki wametoa
zawadi mbalimbali kwa wagonjwa hao kwa ajili ya kufurahia sikuku hiyo ya Pasaka
ambayo inapewa umuhimu mkubwa na wakristo wote duniani.
“Benki yetu itaendelea kusaidia
hospitali hii kama njia ya kutoa mchango kwa jamii,” alisema.
kwasasa hospitali hiyo inajenga kituo
kikubwa cha mama na mtoto.
Naye
Meneja Mawasiliano ya Ndani wa hospitali hiyo ya CCBRT, Bw. Abdul Kajumulo aliishukuru
kwa kuwa mstari wa mbele katika kutoa misaada mbalimbali.
“Tunaishukuru
benki kwa kuja leo hii kula chakula cha pasaka na wagonjwa wetu,” alisema na kuongeza kusema kuwa wadau wengine
wanahitajika kuiga mfano huo.
Alisema
hospitali hiyo inatoa huduma ya afya katika magonjwa ya macho,fistula na mifupa.
Alisema
hospitali inafanya kazi kwa kushirikiana na Serikali na mashirika ya kimataifa
katika kuhudumia jamii ya watanzania.
Mmoja
wa wagonjwa aliyeshiriki chakula hicho, Bi. Shida Khamis kutoka Mkoa wa Dodoma
alisema anaishukuru benki hiyo kwa kuwakubuka kula chakula cha pasaka pamoja
nao.
Alisema
watanzania na mashirika mbalimbali yanahitajika kuiga mfano wa benki hiyo
katika kusaidia hospitali hiyo na watu wenye matatizo.
Huu ni mwaka wa nne tangu Benki ya
Afrika Tanzania ilipoanza kushiriki na wagonjwa sikukuu ya pasaka.
Mwisho
No comments:
Post a Comment