Thursday, July 24, 2014

Benki ya BOA yavutiwa na uvumilivu wa kidini Tanzania

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Afrika Tanzania Bw. Ammish Owusu – Amoah akizungumza na viongozi mbalimbali kutoka katika jumuiya za kiislamu, makampuni pamoja na wateja wa benki hiyo wakati walipoandaa futari , katika Hotel ya Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni kujumuika pamoja na kuzungumza nao wakati wa kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa ramadhani ambapo waislamu  duniani kote wakiwa huwa kwenye  mfungo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Afrika Tanzania Bw. Ammish Owusu – Amoah (kulia) akizungumza jambo na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bw. Juma Reli, muda mfupi mara baada ya kupata futari iliyoandaliwa na Benki hiyo kwa wateja wake mbalimbali, katika Hotel ya Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni kujumuika na wateja wao pamoja na viongozi kutoka jumuiya  mbalimbali za kidini wakati wa kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa ramadhani ambapo waislamu  duniani  kote wakiwa huwa kwenye mfungo.
Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI Mtendaji wa BANK of Africa Tanzania , Bw. Ammish Owusu-Amoah, amezungumzia  amani, umoja, upendo, mshikamano wa  pamoja na kutokua na ubaguzi wa dini ni vitu pekee vilivyochangia kujenga uchumi imara na kuleta maendeleo  miongoni mwa  watanzania.

“Ninastaajabu sana kuona  dini hapa Tanzania zinawavuta watu pamoja badala ya kuwagawanya kama ilivyo sehemu nyingine duniani,”  Bw. Owuso-Amoah alitoa dukuduku hiyo  jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na viongozi mbalimbali kutoka katika jumuiya za kiislamu, viongozi kutoka  makamuni mbalimbali na wateja wa benki hiyo wakati  futari jioni iliyoandaliwa na benki juzi usiku.

Amesema anatambua kuwa ramadhani ni kipindi ambacho waislamu wanafunga  kwa ajili ya kufanya toba na kuomba kwa ajili ya wale wenye shida na kuonyesha upendo hata kwa wale ambao ni maadui zako.

“Watanzania hawana budi kulinda na kuimarisha  misingi ambayo imeshajengwa  ya kuendelea kuheshimiana na kushirikiana kwa madhehebu ya dini zote bila kubaguana,” alisema.

Bw.Owusu-Amoah ambaye pia raia wa Ghana, alisema anashangaa kuona jinsi gani wanatanzania wanashirikiana na kuweka kando tofauti zao za kidini jambo ambalo inabidi kuingwa katika sehemu nyingine katika bara la Afrika.

Ameongeza kuwa wao kama benki wameliona hilo na kuamua kuwakutanisha watu ili kula nao pamoja katika kipindi hiki ili kuendeleza umoja, amani na  mshikamano uliopo miongoni mwa watanzania

Kwa upande wake Sheikh Issa Othman Issa wa msikiti wa Mansour ulioko upanga jijini Dar es Salaam, amesema siku 29 walizofunga wameweza kujizuiya hivyo ni vema wakatumia fursa hiyo kujizuiya mwaka mzima ili kuendelea kupmpendeza mungu kwa yale mazuri.

Ameongeza kuwa kipindi hiki kimekua ni kipindi cha kheri kutokana na watu wengi kuwa karibu na familia zao na hivyo kusaidia kuongeza upendo katika kaya mbalimbali ndani na nje ya nchi.

“Kipindi hiki cha mfungo ni kipindi muhimu sana kwa waislamu kati kutekeleza na kulinda nguzu muhimu ya dini ya kiislamu,” alisisitiza na kusema kuwa Watanzania ni wamoja siku zote.

Hafla hiyo ya futari iliyofanyika kwenye Hotel ya Kililimanjaro Hyatt Regency ilihudhuriwa pia na Naibu Gavana wa Benki Kuu, Bw. Juma Reli.



Mwisho.

DART yawataka wanaofanyia biashara kwenye miundominu ya mradi kuondoka

Mshauri mkuu wa Ufundi wa Wakala wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka ( DART) Bw. Dieter Schelling(katikati) akijadidiliana na  Mkurugenzi wa Usafiri na Mipango wa Wakala, Mhandisi Serapion Tigahwa (kulia) na Meneja wa Usalama Barabarani wa Wakala, Mhandisi Mohamed Kuganda (kushoto) jana   wakati walipofanya ukaguzi wa kutenmbelea baadhi ya maeneo ya mradi huo katika barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam jana ili kujionea maendeleo ya mradi huo ambao unatarajia kukamilika  hivi karibuni  na kukabidhiwa kwa serikali.
Mshauri mkuu wa Ufundi wa Wakala wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka  (DART) Bw. Dieter Schelling (katikati) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Usafiri na Mipango wa Wakala, Mhandisi Serapion Tigahwa (wapili kulia), Afisa Mipango Miji wa Wakala, Bw. Edwin Kema (kulia), Meneja Usalama wa Barabara wa Wakala, Mhandisi Mohamed Kugando (wa pili kushoto) na Ofisa Uhjamishaji Makazi, Bw. Deosdedit Mutasingwa (kushoto) ukaguzi wa kutembelea baadhi ya maeneo ya mradi huo katika barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam jana hali ya mwenendo mzima wa maendeleo ya mradi huo ambao unatarajia kukabidhiwa hivi karibuni kwa serikali, kulia ni Mkurugenzi wa usafirishaji wa Dart Mhandisi Tigahwa Serapion. 
Baadhi ya wafanyabiashara ndogondogo wakiendelea kufanya biashara katika kituo cha mabasi madogo ubungo jijini Dar es Salaam, licha ya kupewa amri ya kuondoka katika ili kuepusha uharibifu wa miundombinu ya barabara inayoendelea kujengwa katika eneo hilo, ambalo kwa sasa limegeuzwa na wafanya biashara kuwa soko na kusababisha usumbufu kwa mafundi wa kampuni ya ujenzi ya Strabag.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Wakala wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) umewataka  wafanyabiashara wanaotumia  maeneo ya miundombinu yaliyojengwa kwaajili ya watembea kwa miguu na baiskeli kufanyiabiashara zao kuondoka maramoja  kabla ya hatua za kisheria hazijafuata.

Aidha Wakala amewataka wafanyabiashara hao kwenda kwenye maeneo ambayo serikali imeyatenga kwaajili ya kufanyiabiashara baadala ya kuvamia maeneo ambayo yamejengwa kwaajili ya mabasi yaendayo haraka.

Hatua hiyo imekuja baada ya timu ya maafisa kutoka  kwa Wakala  kufanya ukaguzi wa kuangalia maendeleo ya mradi huo umbao kwa sasa upo katika hatu za mwisho kabla  Mkandarasi haujaukabidhi rasmi kwa serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la kimara jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Usafirishaji na Mipango wa  DART,  Mhandisi  Serapion Tigahwa,  alisema ni vyema wananchi na wafanyabiashara wakatambua kuwa serikali haimkatazi mtu kufanya biashara lakini yapo maeneo maalumu yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli hizo.

“Tunatambua kuwa watu wanajitafutia kipato lakini zipo sehemu zilizotengwa na mamlaka husika kwa ajili ya kufanyiabiashara,” alisema Mhandisi Tigahwa na kuongeza kuwa ni vyema wafanyabiashara wakaondoka kwa hiari yao sasa kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa.

Alisema kmebakimiezi michache ili mradi huo uweze kukabidhiwa na kuanza kufanya kazi, hivyo ni jambo la aibu kuanza kuharibu mundombinu na kufanya kazi kinyume na matarajio yaliyokusudiwa.

“Barabara hizi zimejengwa kwa ajili ya mabasi yaendayo haraka na si vinginevyo” alisisitiza Tigahwa na kuongeza kuwa maeneo yaliyojengwa kwaajili ya watembea kwa miguu yamegeuzwa sehemu za kuegesha pikipiki na bajaj.

“Hatuwezi kuvumilia hali hii ya uharibifu na matumizi hovyo ya miundombinu kwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mtu yeyote atakaye kiuka maagizo hayo na kuendelea kubaki katika maeneo ya mradi basi hatua kali zitachukuliwa,” alisema.

Aliongeza kuwa serikali imetumia gharama kubwa kutekeleza mradi huo wa mabasi yaendayo haraka hivyo ni vema wananchi wakaunga mkono juhudi hizo kwa kuihafadhi na kuilinda miundombinu iliyopo.

“Tunaomba wananchi wainge mkono serikali kwa juhudi hizi inazozifanya kwa kuitunza na kuilinda miundombinu hii,” Mhandisi Tigahwa alisisitiza.

Mhandisi Tigahwa a aliwataka pia  wananchi kuacha tabia ya kutupa taka hovyo katika barabara hizo za mabasi yaendayo haraka, huku akiongeza kuwa vitendo hivyo si vya kiungwana na ni aibu kwa Taifa.

“vitendo kama hivi kwa kweli ni aibu, na wanaotupa taka si watoto bali ni watu wazima naomba waache tabia hiyo Mara moja,”alisema

Kwa upande wake, Mshauri Mkuu wa Ufundi wa DART, Bw. Dieter Schelling ambaye alikuwepo kwenye ziara hiyo ya kukagua maendeleo ya mradi alisema jitihada za makusudi lazima zifanywe au kuchukuliawa ili kulinda miundombinu ya maradi.

“Barabara za watembea kwa miguu lazima ziheshimiwe nazipo siyo kwa ajili ya maegesho ya pikipiki, bajaj na kufanyia biashara,” alisema na kutaka wavazi wote kwenye miundombinu ya mradi kuondolewa.

Bw. Schelling pia amewaomba madereva kuwa wangalifu wawapo katika barabara ya mabasi yaendayo haraka ili kuepusha uharibifu wa miundombinu kwenye eneo la mradi jambo ambalo litasaidia kudumu kwa muda mrefu kwa miundombinu ya barabara hizo.

Mwisho.